Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Butiama, Mkoani Mara Solomoni Ngiliule kutokana na kushindwa kutimiza majukumu yake kama Mkurugenzi.
Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Seleman Jafo ametangaza uamuzi huo wa rais, leo Jumanne Januari 23, ambapo pamoja na mambo mengine amemtaka Katibu Mkuu wa Tamisemi kumchukulia hatua stahiki kwa mweka hazina wa Halmasahuri ya Wilaya ya Butiama ambaye alikuwapo wakati matumizi mabaya yalipokuwa yanatokea.
“Katika ziara yangu Mkoa Mara, nimekutana na wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo lakini katika ziara hiyo imebainika wazi kuwa wako watendaji katika mamlaka ya Serikali za Mitaa ambayo wamepewa katika kuwatumikia wananchi.
“Kutokana na mambo mbalimbali yalitojitokeza Mkoa wa Mara, rais ambaye pia ndiye waziri mwenye dhamana Ofisi ya Tamisemi amechukua fursa hiyo baada ya yaliyojiri mkoani hapa rais ametengu uteuzi huo wa Ngiliule kuanzia leo hii,” amesema Jafo.
Hata hivyo, Jafo amewataka watendaji wote kuhakikisha wanatimiza makujukumu yao kwa dhamana kubwa waliyopwa kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania wanachukua majukumu yao na wafahamu kwamba kwa kupitia majukumu hayo serikali imewekeza rasilimali fedha nyingi katika maeneo hayo ikiwamo kupitia bajeti ya nchi.
“Tutawachukulia hatua watendaji hao watakaoshindwa akutimiza majukumu yao kama wa Butiama na wengine watimize majukumu yao,” amesema.