29.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

JPM AKUTANA NA WATEULE WAKE

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM


Dk. John Magufuli
Dk. John Magufuli

RAIS na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi watatu wa CCM, aliowateua hivi karibuni kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika safu ya uongozi ngazi ya taifa.

Viongozi hao ni Naibu Katibu Mkuu Bara, Rodrick Mpogolo, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Siasa na Mambo ya Nje, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, ilisema baada ya mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, jana, Polepole alisema lengo la mazungumzo hayo ilikuwa ni kumweleza Mwenyekiti wa CCM fikra na mipango ya awali na namna walivyojipanga kwa kushirikiana na viongozi wengine wa chama, kusimamia na kutekeleza ajenda ya mageuzi ndani ya chama ambayo msingi wake ni kuirejesha CCM kwa watu.

“Na Rais ametuhakikishia kwa asilimia 100 kwamba msimamo wa kufanya mageuzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi ni kukirudisha kwenye misingi ambayo chama hiki kilianzishwa, yaani chama cha wanyonge na chama ambacho kinajinasibu na shida za watu, unatekelezwa.

“Ametuambia tukafanye kazi kwa bidii, Watanzania wana matumaini makubwa sana na Chama Cha Mapinduzi na sisi tumemhakikisha kwenda kuchapa kazi ili dhamira ya kujenga Tanzania mpya iweze kuakisiwa na kuletwa na CCM mpya,” alisema Polepole.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles