31 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 3, 2023

Contact us: [email protected]

KINARA WA UTAPELI AKAMATWA DAR

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


acp-advera-bulimbaJESHI la Polisi linamshikilia mkazi wa Buza, wilayani Temeke, Dar es Salaam, Wilfred Masawe (36), kwa tuhuma za utapeli.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi hilo, ACP Advera Bulimba, imesema mtuhumiwa huyo alitumia mbinu mbalimbali kuhalalisha utapeli wake zikiwamo za kujifanya kama kiongozi wa Serikali.

“Kwa kutumia mtandao wa WhatsApp, mtuhumiwa alidai kuwa yupo nje ya nchi na kuna msiba ambao umetokea nchini unaomuhusu, hivyo alikuwa akitoa maelekezo kwa watendaji wa Serikali waweze kusaidia gharama za matibabu hospitalini, gharama za kusafirisha mwili wa marehemu na gharama za mazishi,” alisema Advera.

Alisema kuwa Masawe alitumia mbinu ya kujifanya askofu na kuomba  michango ya kufanikisha kongamano ambalo alidai anaandaa.

“Baadhi ya matukio aliyofanikiwa kutapeli ni pamoja na kuwatapeli viongozi wa Serikali, wafanyabiashara, mameneja na wakurugenzi wa taasisi za umma, wanasiasa pamoja na waumini wa madhehebu ya dini,” alisema Advera.

Aidha, alisema matukio yote hayo alikuwa akiyafanya peke yake na alikuwa akiyaendesha kwa mawasiliano ya njia ya ujumbe mfupi wa simu (SMS).

Advera alisema jeshi hilo linakamilisha taratibu za kisheria ili mtuhumiwa huyo afikishwe mahakamani sheria ichukue mkondo wake.

“Tunaendelea kutoa tahadhari kwa wananchi wote kuwa makini na mtandao wa matapeli hao na yeyote mwenye  taarifa za matapeli anaombwa kuzifikisha haraka katika kituo chochote cha polisi kilicho karibu ili waweze kushugulikiwa haraka,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles