27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Jose Mourinho ataka kuifundisha Arsenal

MourinhoLONDON, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho amesema hana mpango wa kuondoka jiji la London na kama akiondoka katika klabu hiyo basi atajiunga na klabu ya Arsenal ya jijini humo.

Kocha huyo bado ana imani ya kuendelea kuifundisha Chelsea kwa muda mrefu, japokuwa klabu hiyo imeanza vibaya katika michuano ya Ligi Kuu nchini England, hata hivyo, anaamini kuwa anaweza kuwa kocha wa Arsenal baada ya Arsene Wenger kuondoka.

“Ngoja niweke wazi, ipo siku nitakuja kuondoka Chelsea na kama itakuwa hivyo basi nitaendelea kuishi jijini London.

“Kuna nafasi nyingi za kuwa kocha katika klabu za London kama vile Fulham, QPR, West Ham, Tottenham Spurs, timu ya taifa ya England na klabu ya Arsenal,” alisema Mourinho.

“Lakini kati ya timu hizi zote kuna uwezekano wa kujiunga na klabu ya Arsenal au timu ya taifa ya England,” aliongeza Mourinho.

Mourinho hana uhusiano mzuri na Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, waliwahi kushikana mashati mwaka jana katika mchezo wa Ligi Kuu nchini England, ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles