27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

JOPO LABARIKI KIJANA MREFU KUTIBIWA INDIA

Baraka Elias
Baraka Elias

Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM

JOPO la madaktari waliokuwa wanafuatilia matibabu ya kijana mrefu, Baraka Elias (35), hatimaye limefikia uamuzi kwamba aende kutibiwa nje ya nchi.

Uamuzi huo umetolewa kufuatia gharama kubwa za kuagiza kifaa pandikizi (implant) kutoka nje ya nchi, ambacho angewekewa kubadilisha nyonga yake iliyovunjika.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa MOI, Almas Jumaa, alisema Baraka atakwenda kutibiwa nchini India.

“Ili kuwa na uhakika, badala ya kuagiza kifaa kimoja, ilishauriwa viagizwe vifaa ‘special’ vitatu ili tupate kinachomfaa. Ikumbukwe kwamba vifaa hivyo vingetengenezwa kwa maombi maalumu, hivyo gharama ni za juu sana ikilinganishwa na kupelekwa nje ya nchi,” alisema.

Alisema hivyo MOI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, kwa pamoja wamekubaliana Baraka aende kutibiwa nje ili kupunguza mzigo wa gharama.

“Gharama za matibabu zitalipwa na serikali, MOI tulikuwa tunamtibu kama mgonjwa wa msamaha,” alisema.

Awali ilielezwa kuwa MOI ilishindwa kumfanyia upasuaji kijana huyo kutokana na urefu aliokuwa nao.

Ilielezwa kwamba mashine za MOI haziendani na urefu wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles