26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Jokha Kassim, Msaga Sumu jukwaa moja

NA MWALI IBRAHIM
WAIMBAJI wa taarabu, Jokha Kassim na Msaga Sumu, wanatarajiwa kunogesha onyesho maalumu la kundi la taarabu la Wakali wao Modern Taradansa, litakalofanyika Ijumaa hii katika ukumbi wa JM Hotel, Manzese, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kundi la Wakali wao, Thabit Abdul, alisema usiku huo ni maalumu kwa ajili ya kuukaribisha mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, unaotarajiwa kuanza Juni 19.
“Tumewaandalia mashabiki wetu zawadi ya wimbo mpya ambao tutauzindua siku hiyo ambapo mashabiki watapata nafasi ya kuufahamu na kuusikia siku hiyo hiyo,” alisema.
Hata hivyo, sambamba na wasanii, pia wasanii chipukizi watapagawisha onyesho hilo, akiwemo Mc Sudy na Dogo Jack.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles