NA THERESIA GASPER
MWANAMITINDO Jokate Mwegelo amesema ili wanamitindo wadogo waweze kufanikiwa katika kazi zao, lazima wajenge mitandao ya mawasiliano mazuri na watu mbalimbali.
“Msanii unatakiwa kuwa mfano mzuri katika jamii kwa kufanya mambo yanayokubalika ili jamii iweze kukufikiria vizuri na wengine wajifunze mazuri kupitia wewe,” alisema Jokate, katika kongamano la Jukwaa la Sanaa lililofanyikia jana kwenye ukumbi wa BASATA, jijini Dar es Salaam.
Naye mwanamitindo Asia Idarous, alisema kuendekeza kashfa hakuwezi kumjengea msanii kujitangaza vema kibiashara nje ya nchi.
“Ukiwa mwanamitindo unatakiwa ukubalike kwa vitu vizuri, uwe na msaada, uwe mwaminifu, mkweli na pia uwe na uhusiano mzuri na watu,” alisema.