27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

JOKATE ANG’OLEWA UVCCM, KINANA ATOA NENO

NA MWANDISHI WETU-DODOMA


KAIMU Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Shaka Hamdu Shaka, amesema kutenguliwa kwa uteuzi wa Kaimu Katibu wa Uhamasishaji na Chipukizi jumuiya hiyo, Jokate Mwegelo ni maazimio ya Baraza Kuu.

Uamuzi wa kutenguliwa kwa uteuzi huo wa Jokate, umetangazwa jana mjini hapa na Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri James wakati wa kufunga kikao cha Baraza Kuu la jumuiya hiyo, iliyotanguliwa na semina elekezi huku akisisitiza nafasi hiyo itajazwa baadaye.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Shaka alisema Kamati ya Utekelezaji ya umoja huo ilikutana kwa dharura chini ya Mwenyekiti wake Kheri, na kufanya uamuzi huo hatua ambayo ni utaratibu wa kawaida wa vikao vya jumuiya ambapo ajenda inapowasilishwa bila kujali aliyewasilisha ni nani na kikao kinaporidhia inakuwa ni ajenda ya kikao.

“Itoshe tu kusema ni utaratibu wa kawaida ndani ya CCM pamoja na jumuiya zake kufanya mabadiliko ya aina yoyote pale wanapoona inafaa,” alisema Shaka

Jokate ametumikia nafasi hiyo kwa miezi 11 tangu ateuliwe Aprili 24, mwaka jana.

Awali wakati wa vikao hivyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema sifa ya chama na msingi mkuu wa chama hicho ni kuwa na wigo mpana wa demokrasia inayokifanya kiendelee kubaki madarakani.

Alisema kila mwanachama ana haki ya kusikikizwa, kuchagua na kuchaguliwa kwa mujibu wa matakwa ya watu.

Alisema hatua hiyo ni imekifanya CCM kizidi kuwa na nguvu, uhuru wa watu kujieleza bila hofu ndani ya chama na kujijenga katika uimara zaidi mbele ya umma.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akifungua semina elekezi kwa wajumbe wapya wa baraza hilo mkoani hapa.

 

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles