23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

MAJALIWA AWAPA NENO WAFANYABIASHARA

Na Mwandishi Wetu, Ruangwa


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa, amewataka wafanyabiashara wilayani Ruangwa kutumia taasisi za kifedha kukopa fedha kwa ajili ya kukuza mitaji yao.

Aliyasema hayo  jana, wakati akizungumza na wafanyabiashara wa wilaya hiyo.

Waziri Mkuu ambaye yuko wilayani Ruangwa kwa ziara ya kikazi ya siku mbili, alisema ni vema wakatumia taasisi za kifedha zilizopo ili kukuza mitaji yao.

”Naamini sekta ya biashara ni muhimu katika mabadiliko ya maendeleo, wafanyabiashara ni chachu ya maendeleo kokote na Serikali itaendelea kuwaunga mkono,”alisema

Alisema katika kuhakikisha riba zinapungua, Rais Dk. John Magufuli anaendelea kuzungumza na wamiliki wa taasisi za fedha ili waone namna ya kupunguza riba hiyo.

Alisema lengo la Serikali la kuchukua hatua hiyo ni katika kutekeleza mkakati wake wa  kuwawezesha wafanyabiashara ili waweze kupata mikopo yenye riba nafuu.

Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa Wilaya ya Ruangwa, Said Shea amewaomba wafanyabiashara wenzake watumie fursa za maendeleo zilizoko wilayani humo kwa kupanua wigo wa biashara zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles