John Walker azikwa Tanga

0
1081

Joni WokaNA OSCAR ASSENGA, TANGA

MWILI wa aliyekuwa mwanamuziki wa kizazi kipya, Michael Denis, maarufu kwa jina la John Walker, umepumzishwa katika nyumba yake ya milele katika kijiji cha Panga, Kata ya Kingongoi, Wilaya ya Mkinga, Mkoa wa Tanga.

Katika mazishi hayo yaliyofanyika jana, wasanii watatu tu wenye majina makubwa katika muziki huo, akiwemo Mkoloni, Ras Lion na Dk John, ndio waliofika hadi mwisho wa safari ya aliyekuwa mwanamuziki mwenzao huyo.

Wakati mazishi yakiendelea baadhi ya wasanii  waliojitokeza kuusindikiza mwili huo wa John Walker ulioagwa Muhimbili hawakufika kumzika baada ya kuishia Tanga mjini kwa shughuli zao binafsi.

Ras Lion aliwaomba wasanii wakongwe katika muziki huo waonyeshe upendo kwa kushiriki katika matukio kama hayo badala ya kudharau.

John Walker alifariki dunia baada ya kuangukiwa na kitu kizito wakati alipokuwa akitengeneza gari maeneo ya Sinza, jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here