26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Johari amkana Ray

johariNA SHARIFA MMASI
MMILIKI wa kampuni ya filamu nchini ya ‘RJ Company’, Blandina Chagula ‘Johari’, ameibuka na kushangaza wengi kwa kauli yake kwamba hakuwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji mwenzake, Vicent Kigosi ‘Ray’.
Msanii huyo aliwahi kukiri kuwa na uhusiano huo na msanii huyo na kwamba walishaachana kwa amani, ndiyo maana waliweza kuendelea na kampuni yao ya masuala ya filamu ya Rj Company.
Juzi Johari aliliambia MTANZANIA kwamba, muda mrefu alikuwa akisikiliza wanaodai hana uelewano mzuri na Ray kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji Chuchu Hans na sasa ameamua kuweka wazi suala hilo.
“Ni kwa kipindi kirefu sana yamezuka maneno yanayodai mimi na Ray tulishawahi kuwa wapenzi, kitu ambacho si cha kweli, tena kibaya zaidi wameongeza kuwa hatuna maelewano mazuri kikazi,” alieleza Johari.
Aliendelea kufafanua: “Sikuwahi kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi kama wengi wanavyofikiria na kama ningekuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ray na tumeachana, hata kampuni yetu ingeshavunjika kwa kuwa tungekuwa na chuki, nawaambia hatutegemei kutengana kikazi wala kirafiki,” alisema Johari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles