26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

JK: Kustaafu kwangu si mwisho wa kuwatumikia Watanzania

Na GUSTAPHU HAULE – PWANI


RAIS mstaafu Jakaya Kikwete amesema kustaafu kwake si mwisho wa kuwasaidia wananchi, kwa sababu kwa sasa bado anaendelea kutimiza wajibu wake wa kulitumikia taifa kama Mtanzania.

Pia amewataka wastaafu wa kada mbalimbali hapa nchini, hususani wa kada ya afya, kuendelea kutumia taaluma zao kuwahudumia Watanzania kama ambavyo anafanya na kwamba kustaafu katika utumishi isiwe mwisho wa kusaidia jamii.

Akizungumza mjini hapa jana katika kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha, alisema yeye alistaafu kazi na hakustaafu kufikiri.

Alisema mahitaji ya huduma kwa jamii, hususani katika sekta ya afya bado ni makubwa na mategemeo ya wananchi yapo kwa wauguzi, madaktari na wakunga, hivyo ni vyema wataalamu wa afya wanaostaafu wakaendelea kutoa huduma maeneo yao wanayoishi.

“Nitoe wito kwa wastaafu kuendelea kutumia …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles