30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

JK awashukia mabalozi

Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete

NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

RAIS Jakaya Kikwete amesema kuna ushahidi unaothibitisha baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini,wamekuwa wakichaganya dini na siasa na hata kutumia udini kuunga mkono shughuli za baadhi ya vyama vya siasa.

Kutokana na hali hiyo, amewaomba mabalozi hao kuiokoa Tanzania katika majanga makubwa yanayoweza kuipata kwa kutumia dini kuendeleza siasa, hatua ambayo amesema ni ya hatari.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi wakati wa chakula cha usiku na viongozi wa dini nchini ambao wanaendelea na mkutano wao wa mwaka kwenye Hoteli ya White Sands, Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku nne ulioanza juzi unaojulikana kama Tanzania Christian & Muslim Religious Leaders’ Initiative for Peace and Co-existence ni mwendelezo wa mikutano ya viongozi wa dini kubwa za Kikiristo na Kiislamu kwa lengo la kujenga na kuleta amani na maelewano nchini.

Rais Kikwete aliungana na Mshauri Mkuu wa Taasisi ya Programme for Christian-Muslim Relations in Africa (PROCMURA)  ambaye alionya kuhusu hatari inayoweza kuikabili dunia kwa sababu ya kuingiza dini katika siasa.

“Mwakilishi wa PROCMURA ametoa ujumbe mzito sana. Ametoa fumbo ambalo amewaasa mabalozi wasiingize dini katika siasa na wasiingize siasa katika dini.

“Na mimi nataka kuungana naye na kuwaomba mabalozi waiokoe nchi yetu katika majanga makubwa yanayoweza kutokea kutokana na kutumia dini kuendeleza siasa. Ni njia ya hatari kweli kweli.

“Kuna ushahidi sasa kuwa baadhi yetu, baada ya kushindwa kutumia ukabila katika kuendeleza siasa, sasa tumegeukia dini. Mnatumia dini kuunga mkono baadhi ya shughuli za kisiasa na baadhi ya vyama vya siasa,” alisema Rais Kikwete.

Mkutano huo unaodhaminiwa na Taasisi ya Programme for Christian-Muslim Relations in Africa (PROCMURA) yenye makao yake makuu jijini Nairobi, Kenya, unahudhuriwa na mabalozi 15 wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, mashirika kadhaa ya kimataifa na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika mkutano huo ni wa Ujerumani, Iran, Marekani, Norway, Uturuki, Sweden, Canada, Denmark, Finland, Misri, Qatar, Uswisi, Palestina, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Saudi Arabia na Umoja wa Ulaya (EU).

Viongozi wa dini wanaoshiriki katika mkutano huo wanatoka Zanzibar, Dar es Salaam, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Lindi, Arusha, Geita na Mbeya.

Mwisho

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. kuzungumzia kitu ambacho hakipo katika jamii yetu ni uchochezi pia, kwani ni njia kutengeneza ufitini miongoni mwa watu. nijuavyo mimi hakuna mtu yeyote anayejihusisha na kazi ya kuwafarakanisha watanzania kwa misingi ya dini au kabilaa isipokuwa watawala wakiona mtu anajitahidi kuwaelimisha watanzania juu ya haki zao za msingi huambi huambiwa anafanya uchochezi ili kuwatisha. tanzania ya leo si ile ya zamani,\

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles