25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

JK afanyiwa upasuaji wa tezi dume

Jakaya Kikwete in USNA FREDY AZZAH, Dar

RAIS Jakaya Kikwete, amefanyiwa upasuaji wa tezipdume (prostrate) katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyopo Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.

Taarifa zilizotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu  jana, zilisema upasuaji huo ulifanyika alfajiri ya Novemba 8, mwaka huu.

“Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.

“Upasuaji huo uliofanyika alfajiri na kuchukua saa moja nusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa. Hali ya mheshimiwa rais inaendelea vizuri, bado yuko wodini akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari na kupatiwa tiba.

“Wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais Kikwete kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana,” ilisema taarifa hiyo.

Tezi dume ni nini

Tezi dume ipo kwa mamalia wa kiume na ina umbo kama yai (oval shape) na upana CM 4 na unene CM 3 ingawa vipimo hivi madaktari wanasema vinatofautiana kwa kila mwanamume.

Tezi dume inazunguka shingo ya kibofu cha mkojo na kuzunguka mrija unaopeleka mkojo nje (urethra).

Kwa kawaida tezi hii inauombo la wastani na huongezeka ukubwa kadri ya umri wa mtu unavyosogea.

Dk. George Mbaga kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anasema tezi hii hutengeneza majimaji yenye rutuba ya mbegu za kiume.

“Kuna kifuko kiko kwenye kimrija cha mkojo kwa kiingereza tunakiita prostate gland, hicho kifuko kiko kwenye mrija wa mkojo, mwanamume anapofanya mapenzi, manii yakitoka, kimfuko hicho kinatoa maji ya kuzirutubisha.

“Utafiti unaonesha ukifika miaka 50 kwenda juu, kile kimfuko kinakua kupita kiasi, mkojo unakuwa hautoki vizuri, unajisikia kweli haja ndogo lakini ukitaka kujisaidia mkojo hautoki au unatoka kidogo sana.

vipimo

Dk. Mbaga alisema miongoni mwa vipimo ni pamoja na kile cha damu ambacho kitaalamu kinajulikana kama Prostate Specific Antigen (PSA).

Anasema kipimo hicho kinasaidia kutofautisha kati ya saratani ya tezi dume na BPH.

“PSA ni aina ya protini inayozalishwa na seli za tezi dume na kiwango chake huongezeka iwapo mtu anatatizo na kufikia zaidi ya 500.

“Kipimo kingine ni Rectal Ultrasound, kipimo hiki hufanyika iwapo daktari atahisi kuwepo kwa saratani ya tezi dume badala ya BPH.

“Ultrasound ya puru pamoja na kuonyesha taswira ya tezi dume ilivyo, pia humwezesha daktari kuchukua kinyama (biopsy) kwenye tezi dume kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kutofautisha kati ya saratani na BPH,” anasema.

- Advertisement -

Related Articles

3 COMMENTS

  1. Tukisema utawala wa C. C. M haujafanya lolote la maana baadhi ya watu wanaofaidika nao wanakuja juu.Kitendo cha Rais Kikwete kutibiwa ugonjwa huu mdogo huko Marekani ni ushahidi tosha kuwa katika kipindi cha miaka zaidi ya 50 ya uhuru nchi yetu haina cha kujivunia katika huduma za kiafya.Yaani hata Muhimbili haina uwezo wa kutibu ugonjwa huu uliokuwa unamsibu Rais.

  2. Daktari aliyemfanyia upasuaji Rais Kikwete Marekani Ni kijana mdogo Sana kwa umri.Ni fahari kubwa kwa nchi ya Marekani kuwa na mifumo ya elimu yakuwandaa vijana wao kuwa na ujuzi na hadhi ya kumfanyia operesheni rais wa nchi. Bila shaka kombi alizosoma daktari huyu ni PCB. Je, viongozi wa Tanzania hawoni aibu kwenda kutibiwa nje ya nchi wakati nchi yetu Ina raslimali kuzidi Marekaini? Au sisi ni vilema tunaye hitaji msaada badala ya kujitegemea? Je, wanachi tuliomaskini wa kipato tukipata ugonjwa kama huu tutaweza kwenda nje ya nchi kutibiwa? Mbona tukiwa makini tunaweza na sisi kujenga hospitali kama za Marekani na kusomesha watoto wa PCB tukawa tunatibiwa wote hapahapa Tanzania? Hii ni aibu jamani kubwa sana kubisha hodi kwa jirani kujieleza na kuomba omba msaada. Tubadilike viongozi wetu chose chonde.

  3. Kwanza natoa pole kwa rais wangu Jk kwa maradhi Mungu atakusaidia upone haraka uendelee na majukumu yako ya kitataifa na kimataifa, lakini suala la pili kwa mujibu wa wataalam waliobobea kwenye sekta ya utabibu wanasema matadhi ya tezi dume yanatibika hapa nyumbani hivyo naonelea ingekua vizuri kama mh Rais angetibiwa hapa nyumbani ili kuvutia juhudi za serikali yake za kuboresha sekta ya afya kwa ajili ya Watanzania. Tunaona mfano wa aliyekuwa rais wa Afrika kusini hayati Mandela it makes sense

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles