27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

JIONEE TOFAUTI! Mastaa waliowageuza wenzi wao Video Vixen

Diamond akiwa na Zari
Diamond akiwa na Zari

NA CHRISTOPHER MSEKENA,

VIDEO Vixen hupamba vichupa vya nyimbo za wasanii wengi duniani. Utamu wa video kali, pamoja na mambo mengine, lazima iwe na Video Queen mkali / wakali ambao watainogesha.

Hii ndiyo sababu kampuni zinazozalisha mamodo na kufanya wawe lulu mbele ya macho ya wasanii wa Afrika zimeongezeka. Ni kweli kwamba kwa sasa, wadada hawa wamekuwa dili sana kwa wasanii.

Hapa +255 – Bongo Dar es Salaam, wapo wengi, lakini kuna wasanii ambao wameamua kuwaacha wakati fulani na kuwatumia wapenzi / wenzi wao kama walivyofanya mastaa wa mbele, Chris Brown kwa  Karrueche Tran na Tyga kwa Kylie Jenner.

Swaggaz imekuandalia listi ya wasanii hao, ndani na nje ya Bongo (Afrika) ambao wameamua kuwashirikisha ubavu wao kwenye kazi hiyo ambayo kwa sasa inachangamkiwa na mamodo wengi.

ICE PRINCE, Maima – Feelings

Rapa huyu mwenye heshima nchini Nigeria, hapindui mbele ya mrembo Maima Nkewa. Uhusiano wao unafuatiliwa zaidi nchini humo kwa kuwa una nguvu na umedumu kwa muda mrefu. Wana mtoto wa kiume aitwaye Jamal.

Kama hufuatilii Hip Hop unaweza usimfahamu, kwa wasiomkumbuka,  Ice alishirikishwa na  Jokate Mwegelo kwenye ngoma yake ya Leoleo. Ice Prince alipofikiria kuachia kichupa cha ngoma yake ya Feelings, hakutaka kujisumbua zaidi ya kumpachika mpenzi wake Maima katika video hiyo.

JUX, Vanessa – Sisikii

Jux anasema ukitaka yeye na Vanessa uwakutanishe kwenye jukwaa moja basi watataja dau kubwa ili zoezi lako lishindikane. Ndivyo walivyojiwekea utaratibu wa kutochanganya mapenzi na kazi ili watu wasije kupata utajiri kwa mwamvuli wa penzi lao ambalo wiki hii limetawala mitandao ya kijamii kufuatia kwenda kula bata kwenye mbuga ya wanyama huko Serengeti.

Vanessa alilipwa mkwanja wa maana na mpenzi wake Jux pale alipoombwa kushiriki kwenye video ya Sisikii iliyofanyika mwaka jana huko China na kuongozwa na mkali Zed Benson.

Mtiririko wa visa na matukio ndani ya video hiyo unamfanya awafunike mavideo vixen wengine na huenda asingetumika yeye basi video hiyo ingekosa mvuto kwa mashabiki.

WIZKID, Tania Omatayo – Sade

Huyu ndiyo staa wa kwanza Afrika kutokea kwenye chati za Billibord kule Marekani kupitia kolabo yake aliyofanya na Drake. Miongoni mwa kazi zake poa zilizompa kiki kwenye muziki wa Afrika ni Sade ambapo mpenzi wake Tania Omatayo ametumika kama video vixen na akafanya vyema.

BARNABA, Zuuna – Wahalade

Tukirudi Bongo tunadondoka pale Kinondoni Komakoma ndani ya studio za High Table Sound na kumkuta mwanamuziki Barnaba Elias ‘Classic’  ambaye yupo kwenye uhusiano wa muda mrefu na mrembo Zuuna au mama Steve.

Moja ya kitu ambacho huenda hukijui ni kwamba Barnaba amekuwa akipokea simu nyingi za wasanii wa Bongo Fleva wakimtaka amruhusu mpenzi wake kushiriki video zao na hiyo imekuja mara baada ya Mama Steve kuwafunika mavideo vixen kwenye video ya Wahalade.

Barnada anasema alimtumia kwenye video hiyo mara moja tu kwa sababu aliona kwa urembo alionao, angeweza kuvaa uhusika na akapendezesha kichupa hicho – ndivyo ilivyokuwa.

DIAMOND, Zarinah – Utanipenda

Video hii iliyobeba hadithi yenye ujumbe mzito,  ilimlazimu prodyuza God Father kutoa ushauri kuwa wahusika kwenye video hiyo wawe watu wa karibu na Diamond.

Ndiyo maana tukamuona mama yake mzazi, mameneja wake, mtoto wake, wasanii wake, mpenzi wake wa zamani na mhusika mwenyewe ambaye ni Zari.

Kwa nafasi aliyocheza Zari, hakukuwa na ulazima wa kumtumia video vixen mwingine wakati kama urembo na sifa, Zari alikuwa nazo. Video hiyo ilipotoka, iliwashangaza wengi kwa ubora wake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles