MAHITAJI
- Unga wa ngano – vikombe 4
- Maziwa ya unga – vijiko vya supu 2
- Mafuta ya zaituni – kikombe ½
Hamira – kijiko cha supu 1
Chumvi – kiasi
Sukari – kijiko cha chai 1
Maji ya dafu – vikombe 2
Jinsi ya kupika
Changanya vitu vyote katika bakuli na ukande unga. Ufunike na uache uumuke.
Sosi ya Pizza
Kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo – 1
Kitunguu saumu kilichokatwa chembe 3 Sosi ya HP – vijiko vya supu 3
Sosi ya tomato – vijiko vya supu 3
Pilipili manga – kijiko cha chai 1
Oregano – kijiko cha chai ½
Namna ya kutengeneza sosi
Kaanga vitunguu kisha weka kitunguu saumu na vitu vyote iwe sosi.
Epua kwenye moto.
Vitu vya kujaza juu ya pizza
Nyanya zilizokatwa vipande vipande
Pilipili mboga iliyokatwa
Zaituni ikiwa za kijani au nyeusi
Namna ya kutayarisha na kupika
Tengeneza madonge madogo madogo kisha usukume kidogo tu.
Paka sosi juu ya unga.
Weka kiteo upendacho.
Mwagia vitu vya kujaza juu ya pizza,
mwagia cheese kisha pika katika oveni kwa muda wa dakika 20 moto kiasi hadi ziwive.