26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

JINSI YA KUPIKA PIZZA

MAHITAJI 

 

  1. Unga wa ngano – vikombe 4
  2. Maziwa ya unga – vijiko vya supu 2
  3. Mafuta ya zaituni – kikombe ½

Hamira – kijiko cha supu 1

Chumvi – kiasi

Sukari –  kijiko cha chai 1

Maji ya dafu – vikombe 2

 

Jinsi ya kupika

Changanya vitu vyote katika bakuli na ukande unga. Ufunike na uache uumuke.

 

Sosi ya Pizza

Kitunguu kilichokatwa kidogo kidogo – 1

Kitunguu saumu kilichokatwa chembe 3 Sosi ya HP – vijiko vya supu 3

Sosi ya tomato – vijiko vya supu 3

Pilipili manga – kijiko cha chai 1

Oregano – kijiko cha chai ½

Namna ya kutengeneza sosi

Kaanga vitunguu kisha weka kitunguu saumu na vitu vyote iwe sosi.

Epua kwenye moto.

 

Vitu vya kujaza juu ya pizza

Nyanya zilizokatwa vipande vipande

Pilipili mboga iliyokatwa

Zaituni ikiwa za kijani au nyeusi

 

Namna ya kutayarisha na kupika

Tengeneza madonge madogo madogo kisha usukume kidogo tu.

Paka sosi juu ya unga.

Weka kiteo upendacho.

Mwagia vitu vya kujaza juu ya pizza,

mwagia cheese kisha pika katika oveni kwa muda wa dakika 20 moto kiasi hadi ziwive.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles