22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

JET kuadhimisha siku   ya mazingira Rufiji

IMG_0114NA SIDI MGUMIA

CHAMA Cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kesho kitaungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa (UN) kuadhimisha Siku ya Mazingira duniani.

Maadhimisho hayo yatafanyika Mkoa wa Pwani wilayani Rufiji kwa kupanda miti ya Mikoko.

Akizungumzia maadhimisho hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo, alisema wanachama wa JET watashirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rufiji kuhamasisha shughuli za uhifadhi mikoko katika eneo la delta na kufuata shughuli za uvunaji endelevu wa misitu ya asili.

Alisema shughuli nyingine itakayofanyika ni kupanda miti katika Shule ya Msingi Muyuyu iliyopo katika Kijiji cha Muyuyu wilayani Rufiji.

Chikoma alisema maadhimisho ya Siku ya Mazingira, hutoa fursa kwa Serikali, wananchi na wadau wa JET kupima utekelezaji wa maazimio, matamko na mikataba ya kimataifa, kikanda na kitaifa inayohusu maendeleo endelevu na uhifadhi wa mazingira.

“Siku ya Mazingira Duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wananchi wote duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kaulimbiu ya maadhimisho ya siku ya mazingira ya kila mwaka, kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa  na asasi mbalimbali na Serikali kutunza na kuhifadhi mazingira,” alisema Chikomo.

Alisema kaulimbiu ya kimataifa ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani mwaka 2016 kuwa ni ‘mazingira ya asili ndiyo msingi wa maisha bora’ na kitaifa ni ‘tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa kwa kuwa maji ni uhai wa jamii na uchumi wa taifa wakiwemo wanyama.’

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles