Waziri wa Ulinzi nchini Sudan, Ahmed Awad Ibn Auf ametangaza kuwa Rais Omar El Bashir ameondolewa madarakani.
Waziri ametoa tangazo hilo kupitia televisheni na kusema kuwa Bashir yupo na anazuiliwa mahali salama.
Pia ametangaza Serikali ya mpito ya miaka miwili na kueleza kuwa mipaka yote imefungwa na ofisi ya Waziri Mkuu, bunge na usalama wa kitaifa zote zimevunjwa.
Rais El Bashir aliingia madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 na ameliongoza taifa la Sudan kidikteta kwa muda mrefu jambo ambalo limekuwa likipingwa na wengi nchini humo.
Alipochukua madaraka, Sudan ilikuwa katika mwaka wa 21 wa mapigano makali ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Kaskazini na Kusini.