27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

JPM akemea wasambaza pembejeo hewa nchini

Anna Potinus – Dar es salaam

Rais Dk John Magufuli amekemea vikali watu wanaosambaza pembejeo hewa na amewataka waache kufanya hivyo kwa kuwa wanarudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Kauli hiyo imetolewa Aprili 11, kabla ya hajafungua barabara ya Mafinga-Nyigo-Igawa yenye urefu wa kilomita 138.7 katika eneo la mtewele na uwanja wa Polisi –Makambako mkoani Njombe.

“Mtu anadai amesambaza magunia kadhaa ya pembejeo wakati hayapo, hatuwezi tukaendelea na nchi yenye hewa kwa sababu hatuwezi kushiba hewa,” amesema.

“Nilipoingia madarakani niliahidi nitakuwa daktari wa kutumbua majipu zikiwemo hizi hewa ili fedha halali zitumike katika masuala mengine halali, ninajua wapo waliopata pembejeo za haki na tukishamaliza ufuatiliaji wa pembejeo watalipwa,” amesema.

Aidha amewapongeza wakazi wa Mkoa huo kwa ujenzi mzuri wa nyumba ambapo ameitaka mikoa mingine kuiga mfano huo kwa kujenga nyumba nzuri na za kisasa.

“Tangu nimeingia Njombe nimeona nyumba zilizojengwa ni tofauti na nyumba zilizonyengwa huko kwetu kwani hakuna nyumba ya majani zote ni za bati na zimejengwa kwa matofali ya kuchoma ninafikiri mikoa mingine ambayo haijabadilika katika ujenzi wa nyumba waje wajifunze huku,” amesema Dk Magufuli.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles