21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Wabunge: Serikali isitumie polisi kwenye uchaguzi

Maregesi Paul, Dodoma

Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftaha Nachuma (CUF)ameitaka serikali isiwatumie askari polisi wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika baadae mwaka huu.

 Amesema kwamba pamoja na kwamba polisi wanatakiwa kulinda amani, serikali imekuwa ikiwatumia kuharibu uchaguzi na kukipendelea Chama cha Mapinduzi (CCM) na hicho ni kinyume na sheria ya utawala bora ambayo inatambua mfumo wa vyama vingi nchini.

Nachuma pia ameitaka tume ya uchaguzi iwe huru wakati wa chaguzi za serikali za mitaa ili kila chama kishiriki kwa mujibu wa sheria.

 Wakati huo huo mbunge wa Moshi Mjini,Jafar Michael (CHADEMA) amewalaumu wakuu wa mikoa na wilaya kutumia madaraka yao vibaya kwa kuwanyanyasa wapinzani.

Katika hatua nyingine,Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) ameitaka serikali iunde tume kuchunguza malalamiko ya wananchi dhidi ya viongozi wao katika Wilaya ya Chemba.

Wabunge hao wameyasema hayo bungeni leo Aprili 11, walipokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya wizara ya Tamisemi, Utumishi na Utawala bora kwa mwaka wa fedha 2018/19.

- Advertisement -

Related Articles

1 COMMENT

  1. Kwa kweli, viongozi wetu Tanzania wanahitaji kubadilisha mfumo wa usimamizi wa uchaguzi. Malalamiko ni mengi sana kwamba polisi wanaosimamia chaguzi mbalimbali wamekuwa wakitumika katika kubadili matokeo, na wengine wanashutumiwa hata kuondoka na masanduku ya kura na baadaye kurudi nayo yakiwa tayari yana ‘kura zilizopigwa’

    Nashauri kwamba polisi wasitumike katika usimamizi kwenye vituo. Tume ya uchaguzi iajiri vijana ambao hawana kazi (na hao wapo maelfu), kusimama kwenye vituo badala ya polisi. Kama polisi watakaa mbali na vituo, (wakiwa kwenye zile mita mia mbili ambazo wapigakura wanatakiwa wawe) wanaweza kuitwa kirahisi kama litatokea tatizo.

    Jamani tukumbuke machafuko yaliyotokea Kenya miaka kadhaa iliyopita. Tusijidanganye kwamba hata hapa kwetu hayawezi kutokea. Sasa hivi, mioyo ya watu wengi imejaa mawazo kwamba chama tawala kinatumia polisi kugandamiza vyama vya upinzani. Tukumbuke kwamba asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana kwa hivyo ni rahisi sana wao kujihusisha kwenye fujo. Tukiacha hali ya sasa iendelee, tusishangae vijana wa upinzani wakaanza kushambulia wale wa chama tawala baada ya kuhisi kwamba chama tawala ‘kimewadhulumu’ kura zao. Fujo za namna hiyo zikitokea, jeshi la polisi (kwa uchache wa askari walionao) hawataweza kuzizuia. Na hata kama wakija kufanikiwa kuzizima, patakuwa pameshatokea umwagaji wa damu na watu wengine kupoteza maisha. Jamani, nawaombeni sana, sana, sana viongozi wa nchi hii, msikubali tufike huko. Ple-a-se!!!

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles