Maputo, Msumbiji
Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi ametoa ripoti ya Wajeshi wa nchi hiyo kutuliza mashambulizi mapya yaliyofanywa na magaidi wa kundi la kiislamu katika mji kaskazini wa pamla ambapo kuna mradi mkubwa wa gesi unaondeshwa na kampuni ya Total.
Rais Nyusi ameyasema hayo wakati wa mkutano wa chama tawala cha Frelimo uliofanyika Matola, Mkoa wa Maputo.
Mwezi Machi, mamia ya magaidi walio na mafungamano na kundi la Islamic State (IS) walivamia mji huo katika shambulio lililosababisha vifo vya watu nchini humo.
Rais Nyusi alisema tukio la wikiendi lilihusisha jaribio la magaidi kujaribu kuvamia kijiji cha Lumbi, Wilaya ya Palma na pia waliwaua magaidi wenzao watano waliojaribu kujiondoa kwenye kikundi hicho.
Alisema serikali yake iki tayari kuunga mkono msaada wa kigeni kukabiliana na magaidi kaskazini mwa nchi hiyo “hakuna mtu anayepaswa kujiona ana kinga au anaweza kupambana na ugaidi peke yake”.