28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Jermy B Manono, Sharon waachia kitu ‘Asanteh’

KUTOKA Arizona, Marekani mwimbaji wa Injili mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Jermy B Manono a.k.a Lion King, amerudi kivingine na wimbo, Asanteh aliomshirikisha, Sharon.

Akiuzungumzia wimbo huo uliotoka mwishoni 2020, Manono alisema Asanteh ni ngoma ya shukurani kwa Mungu kwa mambo mengi makubwa aliyoyatenda kwa mwaka huo ambao ulikuwa na changamoto nyingi.

“Nashukuru mapokezi yamekuwa makubwa kwenye chaneli yangu ya YouTube tangu nilipouachia wimbo Asanteh, namshukuru pia Sharon kwa kufanya vizuri, mpaka sasa kila mtu anaweza kuingia YouTube ya Jermy B Manono akautazame bila shaka atabarikiwa kwa sababu katika kipindi hiki cha mwaka mpya tunapaswa kumwambia Mungu Asanteh kwa mambo makuu aliyotutendea 2020, naomba mashabiki zangu waendelee kusapoti huduma ninayofanya kwa kusikiliza muziki wangu kwenye platform zote kama iTunes, SoundCloud, Apple Music, Audiomack na wanicheki kwenye mitandao yote ya kijamii kunipa ushauri na maoni yao,” alisema mwimbaji huyo ambaye ni boss wa By Nation Brand.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles