15.00
Normal
0
false
false
false
EN-GB
X-NONE
X-NONE
Na Derick Militon, Meatu
Zaidi ya wakazi 100,000 wa jimbo la Kisesa katika Wilaya ya Meatu mkoani
Simiyu hawatalazimika tena kutembea umbali mrefu zaidi ya kilometa 100 kufuata
huduma za dharura, baada ya Shirika la AMREF kukamilisha ujenzi wa jengo kubwa
la upasuaji (Theater) katika kituo cha Afya Mwandoya.
Mradi huo ambao umegharimu kiasi cha Sh milioni 140, ujenzi wake umekamilika
kwa asilimia 100 ambapo leo Alhamisi Julai Mosi, 2021 umezinduliwa rasmi na
mbio za Mwenge maalum wa Uhuru 2021 kwa ajili ya kuanza kutumika.
Akisoma taarifa ya ujenzi huo, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Dk. Paul
Masunga, amesema ujenzi wa jengo la upasuaji ulianza Aprili 25, 2019 ambapo
hadi kukamilika kwake, Shirika la Amref Health Africa ndilo limefadhili kupitia
mradi wake wa Uzazi Uzima awamu ya pili.
Amesema kuwa kituo hicho cha Afya kimekuwa tegemeo kubwa kwa wananchi wa
jimbo hilo na maeneo ya jirani.
Amesema kuwa awali wananchi hasa wanawake wajawazito na watoto wenye uhitaji
wa huduma za dharura na wale wenye viashiria vya hatari, walilazimika
kukimbizwa hospitali ya wilaya Mwanhuzi zaidi ya kilometa 50 au hospitali ya
wilaya Bariadi zaidi ya kilometa 50.
Amesema huduma ya upasuaji iliyokuwepo katika kituo hicho ilikuwa ndogo,
ambapo jengo lake lina vyumba vitatu ambavyo ni vidogo, ikilinganishwa na jengo
jipya la Amref ambalo ni kubwa na lenye vyumba vya kutosha.
“Kwa mradi huu huduma zote za dharura sasa zitaanza kupatikana hapa, hii
itasaidia kupunguza mzigo kwa wananchi kutafuta huduma hizi mbali, tutafanya
upasuaji mkubwa na mdogo hapa hapa kituo cha Afya Mwandoya,” amesema Dk.
Masunga.
Dk. Masunga amesema kuwepo kwa huduma za upasuaji kwenye kituo hicho
itasaidia kuongeza utolewaji wa huduma za dharura kwa ufanisi za upasuaji kwa
akina mama wajawazito na wale wenye viashiria vya hatari.
Aidha, amesema kuboreshwa kwa huduma hiyo itaongeza ufanisi wa kutoa huduma
kwa watoa huduma kwenye kituo hicho, kutokana na jengo hilo kutimiza vigezo
vyote muhimu vinavyohitajika katika mtirirko wa kutoa huduma za upasuaji.
Mara baada ya kuzindua jengo hilo, Kiongozi wa mbio za Mwenge, Luten
Josephine Mwambashi, amepongeza ujenzi huo na kushukuru Shirika la Amref kwa
kuwasogezea huduma karibu wananchi.
Mmoja wa wananchi, Rahel Girya ameshukuru Amref na serikali kwa kuwasogezea
huduma za upasuaji karibu, kwani awali ameeleza waliteseka sana kufuata huduma
hizo hospitali ya Wilaya pamoja na Wilaya jirani ya Bariadi.