23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jengo la upasuaji Meatu kuokoa Wananchi kutembea Km 100

15.00 Normal 0 false false false EN-GB X-NONE X-NONE Na Derick Militon, Meatu Zaidi ya wakazi 100,000 wa jimbo la Kisesa katika Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu hawatalazimika tena kutembea umbali mrefu zaidi ya kilometa 100 kufuata huduma za dharura, baada ya Shirika la AMREF kukamilisha ujenzi wa jengo kubwa la upasuaji (Theater) katika kituo cha Afya Mwandoya. Mradi huo ambao umegharimu kiasi cha Sh milioni 140, ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 100 ambapo leo Alhamisi Julai Mosi, 2021 umezinduliwa rasmi na mbio za Mwenge maalum wa Uhuru 2021 kwa ajili ya kuanza kutumika. Akisoma taarifa ya ujenzi huo, Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho, Dk. Paul Masunga, amesema ujenzi wa jengo la upasuaji ulianza Aprili 25, 2019 ambapo hadi kukamilika kwake, Shirika la Amref Health Africa ndilo limefadhili kupitia mradi wake wa Uzazi Uzima awamu ya pili. Amesema kuwa kituo hicho cha Afya kimekuwa tegemeo kubwa kwa wananchi wa jimbo hilo na maeneo ya jirani. Amesema kuwa awali wananchi hasa wanawake wajawazito na watoto wenye uhitaji wa huduma za dharura na wale wenye viashiria vya hatari, walilazimika kukimbizwa hospitali ya wilaya Mwanhuzi zaidi ya kilometa 50 au hospitali ya wilaya Bariadi zaidi ya kilometa 50. Amesema huduma ya upasuaji iliyokuwepo katika kituo hicho ilikuwa ndogo, ambapo jengo lake lina vyumba vitatu ambavyo ni vidogo, ikilinganishwa na jengo jipya la Amref ambalo ni kubwa na lenye vyumba vya kutosha. “Kwa mradi huu huduma zote za dharura sasa zitaanza kupatikana hapa, hii itasaidia kupunguza mzigo kwa wananchi kutafuta huduma hizi mbali, tutafanya upasuaji mkubwa na mdogo hapa hapa kituo cha Afya Mwandoya,” amesema Dk. Masunga. Dk. Masunga amesema kuwepo kwa huduma za upasuaji kwenye kituo hicho itasaidia kuongeza utolewaji wa huduma za dharura kwa ufanisi za upasuaji kwa akina mama wajawazito na wale wenye viashiria vya hatari. Aidha, amesema kuboreshwa kwa huduma hiyo itaongeza ufanisi wa kutoa huduma kwa watoa huduma kwenye kituo hicho, kutokana na jengo hilo kutimiza vigezo vyote muhimu vinavyohitajika katika mtirirko wa kutoa huduma za upasuaji. Mara baada ya kuzindua jengo hilo, Kiongozi wa mbio za Mwenge, Luten Josephine Mwambashi, amepongeza ujenzi huo na kushukuru Shirika la Amref kwa kuwasogezea huduma karibu wananchi. Mmoja wa wananchi, Rahel Girya ameshukuru Amref na serikali kwa kuwasogezea huduma za upasuaji karibu, kwani awali ameeleza waliteseka sana kufuata huduma hizo hospitali ya Wilaya pamoja na Wilaya jirani ya Bariadi.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles