23.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 13, 2024

Contact us: [email protected]

Jengo la Polisi lanusurika kuteketea kwa moto

adveraNa Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

JENGO la Polisi Makao Makuu, jijini Dar es Salaam limenusurika kuteketea kwa moto baada ya kutokea hitilafu ya umeme katika jengo hilo.

Moto huo uliwashtua wafanyakazi wa polisi makao makuu ambao walikuwa wakikimbizana kutoka nje ili kunusuru maisha yao.

Akizungumzia tukio hilo, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba,  alisema moto huo ulianzia katika dari kwenye jengo la ghorofa ya nne ambao baada ya kuanza kuungua moto na moshi kuenea katika baadhi ya maeneo ya jengo hilo.

Alisema wafanyakazi walipoona cheche katika ghorofa hiyo ndipo walipoanza kutoa taarifa kwa wafanyakazi wenzao na kutoka nje ili kujiokoa.

“Moto ulianzia katika dari ambapo kulikua kunatoa cheche nyingi na baadae tumetoa taarifa katika kikosi cha ulinzi na uokoaji zimamoto wamekuja kuuzima,” alisema.

Alisema moto huo haujaleta madhara yoyote kwa wafanyakazi wala katika vitu vyovyote vya ofisi.

“ Tunashukuru kikosi cha zimamoto kufika mapema na kwa wakati hata hivyo watu walikuwa wakisema tulikuwa katika mazoezi lakini si hivyo bali ni moto tu na tayari umedhibitiwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles