25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Serikali yabeba deni la Bodi ya Utalii

maghembeNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii, imejitwisha mzigo wa deni la Sh bilioni 4 ambalo Bodi ya Utalii inadaiwa.

Deni hilo ni  ambalo linahusu matangazo yanayoanzia mwaka 2013/ 2014 ambalo lilikuwa likihusu matangazo yote ya utalii yaliyokuwa yakifanyika ndani na nje ya nchi katika viwanja mbalimbali vya soka vya Ulaya.

Akizungumza na viongozi wa bodi hiyo, jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghebe alisema wizara inachukua jukumu la kulipa deni hilo ili bodi hiyo iweze kufanya kazi kwa amani.

“Deni hilo lisukumiwe wizara ili tulifanyie kazi, kwa kuwa  kama mkiendelea kubaki nalo nyinyi mtashindwa kufanya kazi kwa amani,”alisema Maghembe.

Alisema kutangaza utalii ni zoezi endelevu kwa kuwa ndio chanzo cha mapato kikubwa kuliko sekta yeyote nchini, hivyo aliwataka viongozi wa bodi hiyo kubadili namna ya kufikiri na kutumia rasilimali ilizonazo katika kuwashawishi wawekezeji.

“Lazima tubadili namna ya kufikiri kwa kutenga maeneo mazuri ya uwekezaji na kujitangaza kwa wadau wanaohusika juu ya kujenga hotel kwa vile viwanja tunavyo vya kutosha,”alisema Maghembe.

Pia Maghembe alisema kwamba ni wakati sahihi wa kuwa na mfuko wa kuwawezesha wawekezaji wadogo wa  ndani ili kufika viwango vya kimataifa.

Waziri huyo alisisitiza kwamba mbali na kutoa elimu juu ya wawekezaji hao, bodi hiyo inatakiwa kujitahidi katika miaka miwili ijayo kufikisha watalii milioni 2 badala ya milioni 1 iliyopo sasa.

Aidha Maghembe aliitaka bodi hiyo kuacha kulalamika juu udogo wa bajeti na kuwataka kupanga mipango yao kuendana na kiwango cha fedha walizonazo.

“Serikali ya awamu yatano imedhamiria kupambana na changamoto zinazotokana na watu binafsi, hivyo hakuna haja ya kulalamika juu ya suala la bajeti badala yake ni muhimu kuangalia vipaumbe muhimu ili kuendana na fedha mlizonazo,”alisema Maghembe.

Profesa Maghembe aliitaka bodi hiyo kuruhusu matangazo yote ya utalii yaliyokuwa tayari kuendelea kuoneshwa katika maeneo mbalimbali ndani na nje, huku akiahidi kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza katika bodi hiyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles