Tunu Nassor, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa Bodi ya Waakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), Jenerali mstaafu Davis Mwamunyange, amewataka wananchi wanaohudumiwa na mamlaka hiyo, kuwa na subira wakati serikali ikitekeleza miradi kikubwa ya maji.
Akizungumza katika ziara ya wajumbe wa bodi hiyo kutembelea miradi mbalimbali ya Dawasa, Jenerali Mwamunyange amesema serikali imewekeza miundombinu yenye uwezo mkubwa wa kuweza kuhudumia wakazi wote.
“Kuna uwekezaji wa miradi mbalimbali ya kusambaza maji katika maeneo yote ambayo hayajafikiwa na Dawasa.
“Nawaomba wananchi wa Dar es Salaam na maeneo yote yanayohudumiwa na Dawasa wawe na subira wakati tunatekeleza miradi mbalimbali ya kuwapelekea maji,” amesema Mwamunyange.
Amesema mradi wa ujenzi wa Bwawa la Kidunda uko katika hatua nzuri ambapo utaanza kujengwa hili karibuni.
“Mradi huu utaongeza wingi wa maji katika Mto Ruvu na hivyo kuwa na uhakika wa maji muda wote,” amesema.