Na Victoria Godfrey, Dar es Salaam
Maanda finyu yametajwa kuwa sababu iliyowaangusha kuibuka na Ubingwa Katika mashindano ya Judo ya Afrika Mashariki
yaliyomalizika juzi Visiwani Zanzibar.
Timu ya Tanzania Bara imeshika nafasi ya Pili, huku Kenya wakiibuka na Ubingwa, nafasi ya tatu imeenda kwa wenyeji Zanzibar na Burundi ikimalizia nafasi ya nne.
Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Katibu MKuu wa JATA, Innocent Malya, amesema sababu nyingine ni ukosefu wa ruhusa makazini kwa baadhi ya wachezaji ambao ulichangia kuchelewa kuingia kambini kwa maandalizi.
“Tulichotuangusha kupata Ubingwa ni baadhi ya wachezaji kukosa ruhusa makazini kwao ndio kumechangia ,lakini tumejifunza na tutajipanga upya kwa mashindano yajayo,” amesema Malya.
Malya amesema kuwa ushindani ulikuwa mkubwa kwa timu zote zilizoshiriki kwwnye mashindano hayo, kwani kila mmoja alijiandaa kufanya vyema ili aondoke na Ubingwa.