24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Bongo Open Mind watangaza msimu wa pili wa shindano hilo

Brighiter Masaki

Msimu wa pili wa Shindano la kusaka kipaji cha mtoto la Bongo Open Minds, unatarajiwa kufanyika Juni, Mwaka huu jijini Dar es Salaam likihusisha Mikoa yote nchini.

Akizungumza na www.mtanzania.co.tz jijini Dar es Salaam, mmoja ya Waratibu wa shindano hilo, Mwasisi Kimodoi, amesema kuwa shindano hilo litahusisha watoto wenye umri chini ya miaka 10.

“Mzazi anachotakiwa kufanya mtoto ni kuonyesha kipaji chake alichonacho na kuweza kuwashawishi watu kumpigia kura kwa wingi ili kumsaidia aweze kuwa mshindi katika shindano hilo.

“Mtoto anapaswa kutuonyesha kipaji alicho nacho ikiwa ni kuchekesha, kuigiza, kuimba, kucheza na vingine vingi ambavyo vitawavutia watazamaji na kupigiwa kura,” amesema Kimodoi.

Aidha, ameongeza kuwa mtoto atakayefanya vizuri na kupigiwa kura kwa wingi, atapewa zawadi katika shindano hilo.

“Katika shindano hili mshindi wa kwanza atajinyakulia kiasi cha Sh 600,000, mshindi wa pili Sh 300,000 na mshindi Sh 200,000,” amesema Kimodoi.

Pia katika hatua nyingine Kimodoi amesema shindano hilo litashirikisha Watanzania wote wenye haki ya kupiga kura utofauti wa shindano hilo na kwamba litajumuhisha wote wa nje na ndani ya grupu.

Ili kushiriki shindano

Kimodoi amesema ili Mzazi aweze kumwezesha mtoto wake kushiriki shindano hilo atatakiwa kufanya yafuatayo:

“Mzazi anatakiwa kumrekodi mtoto wake akifanya jambo lolote la kufurahisha na kuelimisha kisha anatuma video na watu wataipigia kura ili kupata mshindi ambaye atakuwa na kura nyingi, nia ni kutaka upigaji wa kura uwe wa haki bila upendeleo unatakiwa kufatilia akaunti za Bongo Open Mind,”amesema Kimodoi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles