30.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

Japanese: Njombe hatuna changamoto ya usafiri

Na Mwandishi wetu,Njombe.

Mwenyekiti wa Umoja wa usafirishaji abiria Mkoa wa Njombe, Daniel Hatanaka (Japanese) amesema mkoa wa Njombe umefanikiwa katika kuingiza magari mapya vijijini tofauti na mikoa mingine ambayo wanapeleka magari mabovu.

Japanese ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa ambapo alisema Mkoa wa Njombe unajitahidi katika ununua magari mapya hatua ambayo imeondoa kabisa cha gamoto ya usafiri kwa wananchi.

“Njombe hatuna changamoto ya magari si mjini au vijijini, ukienda mikoa mingine magari ya zamani ni yaliyotumika kwenye barabara za lami yameisha ndio wanapeleka vijijini,”amesema Japanes.

Hata hivyo, amesema mkoa huo pia hauna changamoto ya usafiri kwani magari yanasubiri abiria na sio abiria kusubiri magari.

Pia amesema ufungaji ving’amuzi kwenye magari yaendayo mikoani umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali na kwamba serikali iongeze juhudi katika kuvisimamia.

‘’Kufungwa kwa ving’amuzi kumesaidia kwa asilimia kubwa kupunguza ajali nchini hata mkoani kwetu hivyo niipongeze serikali kwa hatua hii kubwa, lakini tu waongeze juhudi katika kuvisimamia kwa sababu usimamizi wake si mzuri sana,’’amesema Japanese.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles