23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Jamii yakumbusha kusaidia watoto wenye uhitaji

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya usafirishaji mizigo ya Twalib imetoa msaada wa vyakula katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Alfurqaan kilichoko Chanika jijini Dar es Salaam ili viwasaidi katika kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani.

Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Agnes Kalasan amewaambia waandishi wa habari Aprili 8, kuwa lengo la kufanya hivyo ni kutoa shukurani na asante kwa Mwenyezi Mungu kwa kupitia watoto walio na huitaji katika kipindi hiki cha Ramadhani.

“Watoto hawa wanahitaji vitu vingi ikiwemo nguo, chakula, elimu hivyo tumeona si vyema kumaliza mfungo wa ramadhan bila kuja kuwaona watoto hawa na kuwaletea mahitaji mbalimbali ikiwamo sukari, unga, mafuta ya kupaka, dawa za meno, sabuni za kufulia, na chumvi,” amesema Agnes.

Naye, Nasra Msofe kutoka Taasisi ya Tuamke pamoja Tanzania aliishukuru Serikali kwa kutoa fursa ya elimu bure shuleni katika ngazi ya sekondari huku akiiomba kuibua vipaji vya watoto yatima ili visiishie njiani.

“Huwa tunatembea katika vituo mbalimbali kwa lengo la kwenda kuwasaidia watoto wenye uhitaji hasa watoto ambao hawana wazazi na wanaoishi katika mazingira magumu. Tunaiomba serikali iweze kuibua vipaji vya watoto viliivyopo kwenye vituo hivi ili waweze kujulikana na kusaidiwa zaidi,” alisema.

Naye Mfanyakazi katika kituo hicho, Jumanne Omary amesema ameanza kuishi na kuwalea watoto hao mwaka 2014 hivyo changamoto kubwa aliyokutana nayo kwa watoto hao ni elimu.

“Watoto hawa wanashindwa kufanya mitihani ya kumaliza shule kwa sababu wanakosa pesa na kusababisha kukaa nje bila ya kufanya mitihani. Watoto hawa wapo 75 kati yao 25 wapo sekondari na 50 wapo shule ya msingi na wote ni wakiume,” amesema.

Mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hiko, Jafari Chalamila ameishukuru kampuni hiyo kwa msaada walioutoa na kuwaomba watu wengine mbalimbali wazidi kuwatembelea ili kuendelea kutatua changamoto walizonazo ikiwemo ukosefu wa vitabu, mafuta na vyakula.

Kwa upande wa Mkurugenzi kwa kampuni hiyo, Twalib Hussein ambaye alijumuika na watoto yatima katika hotel ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam, wakati wa futari amesema kuwa ilikuwa ni kiu yake ya muda mrefu kujumuika na watoto wenye huitaji na kupata nao chakula.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles