BAADA ya Real Madrid kupokea kichapo cha mabao 3-2 dhidi ya Sevilla, mshambuliaji wa timu hiyo, James Rodriguez, amesema kuwa hawana wasi wasi na mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya wapinzani wao, Barcelona.
Mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu, ambapo utakuwa El Clasico ya kwanza msimu huu wapinzani hao kukutana.
Barcelona kwa sasa wanaongoza katika msimamo wa Ligi nchini Hispania baada ya juzi kushinda mabao 3-0 dhidi ya Villarreal, wakati Madrid ikiambulia kichapo dhidi ya Sevilla.
“Tunajua wapi tulikosea kwenye mchezo dhidi ya Sevilla, kama mmoja wetu amefunga bao basi tumefunga wote na kama amekosea basi tumekosea wote.
“Hatuna wasiwasi na matokeo hayo, kikubwa ambacho tunakiangalia kwa sasa ni mchezo ujao dhidi ya Barcelona, ila hatuna shaka na mchezo huo japokuwa tumepoteza dhidi ya Sevilla.
“Wao ni Barcelona, tunajua kwamba wapo katika kiwango kizuri, lakini sisi ni Madrid, tunajiamini na mchezo huo utakuwa wa kuvutia,” alisema Rodriguez.