25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Novak Djokovic atwaa taji la Paris Masters

djokovicPARIS, UFARANSA

NYOTA wa mchezo wa tenisi nchini Serbia, Novak Djokovic, amefanikiwa kutwaa taji la michuano ya Paris Masters baada ya kumshinda mpinzani wake, Andy Murray, katika fainali iliyochezwa juzi jijini Paris, nchini Ufaransa.

Nyota huyo namba moja kwa ubora wa mchezo huo duniani, alimshinda mpinzani wake kwa seti 6-2, 6-4 na kufanikiwa kutwaa taji hilo na kumfanya azidi kuweka rekodi mbalimbali.

Djokovic amekuwa mchezaji wa kwanza kuweza kushinda mara sita kwa mwaka michuano ya ATP Masters. Hata hivyo, Murray amempongeza mpinzani wake kwa kuchukua taji hilo na amesema atajipanga kwa ajili ya msimu ujao.

“Amefanya vizuri na ndiyo maana ameshinda, kwa upande wangu hii ni mara yangu ya kwanza msimu huu kuingia hatua ya fainali katika michuano mikubwa kama hii, ninaamini mwakani nitajipanga vizuri kwa ajili ya kupambana na mpinzani wangu.

“Nampa pongezi mpinzani wangu kwa kuzidi kujiongezea furaha kubwa wiki hii, anastahili kuwa namba moja kwa ubora wa mchezo huu,” alisema Murray.

Kwa upande wa Djokovic, amesema amekuwa na furaha kubwa kuchukua ubingwa huo, ila mchezo ulikuwa na ushindani mkubwa, lakini alifanikiwa kuchukua ubingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles