27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

JAMBAZI LADAIWA KUUA POLISI MUSOMA

NA SHOMARI BINDA-MUSOMA


POLISI mkoani Mara, Ephraim Lazaro (G- 1379), ameuawa kwa kupigwa risasi na mtu anayedaiwa kuwa ni jambazi aliyekuwa ametoroka kutoka mahakamani zaidi ya mwezi mmoja uliopita na kufuatiliwa baada ya kupata taarifa zake mahali alipokuwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafar Mohamed, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 7.00 mchana katika Kata ya Buruma wilayani Butiama  ambako askari walikwenda eneo hilo kumfuatilia mtuhumiwa.

Alisema askari wake  alipigwa risasi na jambazi huyo aliyefahamika kwa jina la  Mbogo James, maarufu kwa jina la China.

Alisema jambazi huyo  alikamatwa akiwa na wenzake wawili.

Alisema mtuhumiwa alikuwa akitafutwa baada ya kutoroka mahakamani  akiwa anakabiliwa na kesi ya mauaji na unyang’anyi wa kutumia silaha iliyokuwa ikimkabili.

“Tulipata taarifa za mtuhumiwa huyu na askari wetu walikwenda kumfuatilia eneo husika.

“Kwa bahati mbaya kabla hawajamfikia kumkamata  alikuwa na silaha na alifyatua na kumpata askari wetu ambaye alifariki  dunia muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.

“Jambazi huyu aliuawa akitaka kufanya jaribio la kutoroka na wenzake wawili walifanikiwa kukimbia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles