23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

JALADA MKE WA BILIONEA MSUYA LAITWA KWA DPP

Na KULWA MZEE – DAR ES SALAAM

JALADA la kesi ya mauaji ya kukusudia inayomkabili mke wa bilionea, Erasto Msuya, Miriam Mrina na mwenzake limeitwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hayo yalibainishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita alidai mahakamani kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na jalada limeitwa kwa DPP kwa ajili ya uamuzi wake.

Baada ya kusema hayo Mwita aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Wakili wa utetezi, Peter Kibatala alikubaliana na hoja hizo hivyo mahakama iliahirisha kesi hadi Desemba 11 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni Miriam Mrita na Mfanyabiashara Revocatus Muyella ambapo mara mwisho walifahamishwa kwamba jalada la kesi yao lilishatoka ofisi ya upelelezi Temeke, liko kwa DCI.

Washtakiwa wanakabiliwa na kesi ya mauaji namba 5 ya mwaka 2017,  wanadaiwa kumuua kwa makusudi  Dada  wa marehemu bilionea Msuya, Aneth Msuya.

Watuhumiwa wanadaiwa kufanya tukio hilo Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada, Kigamboni Jijini Dar es Salaam.

Kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa ikiwa imepewa namba 32, ilifutwa Februari 23, 2016 kwa sababu za kisheria.

Baada ya kufutwa washtakiwa walikamatwa tena na kufunguliwa mashtaka upya mashtaka ya mauaji mbele ya Hakimu Simba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles