30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

Jafo awataka Watanzania kutunza mazingira kwa kununua bidhaa rafiki

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Seleman Jafo  amewataka watanzania kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na kununua bidhaa rafiki wa Ozoni (Ozone friendly) ili kulinda tabaka la Ozoni dhidi ya uharibifu.

Waziri Jafo amesema hayo jijini Dodoma Septamba 16, 2021 alipofanya ziara kwenye maduka ya vifaa vya umeme pamoja na mafundi wanaojishughulisha na uuzaji na utengenezaji wa majokofu na viyoyozi katika maadhimisho yakupambana na kulilinda anga la hewa (Ozone layer).

Amesema ozoni ni tabaka la hewa ambalo liko katika anga la juu la pili lifahamikalo kitaalamu kama Stratosphere ambalo linaweka aina ya tabaka ama tambara angani ambalo linazuia mionzi mikali ya jua inayoweza kuleta athari katika afya za binadamu na viumbe hai kuja moja kwa moja duniani.

Amesema kuwa uharibifu wa tabaka la Ozoni unapelekea madhara mbalimbali duniani ikiwemo kuongezeka kwa kiwango cha joto duniani pamoja na kuleta mabadiliko ya tabia ya nchi jambo ambalo ni hatari kwa afya ya binadamu na viumbe hai.

Amewataka Wafanyabiashara kuacha kuuza Majokofu na Viyoyozi vya mtumba kwani vimeonekana kuleta athari kubwa katika vizazi vyetu vya sasa na vijavyo, wafanyabishara wengi wamekuwa wakiuza majokofu ya mtumba yalikuwa yakitumia gesi R 22 ambayo yalikuwa ikiharibu mazingira.

Jafo ametoa wito kwa vijana ambao wanaojishughulisha na masuala ya ufundi wa viyoyozi kwenye Majokofu ya mtumba kutumia aina ya gesi inayoruhusiwa na viwango vya kimataifa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Remidius Mwema ambaye alimwakilisha , Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amesema Dodoma inakuwa kwa kasi hivyo kuna haja ya kutengeneza jukwaa la pamoja litakalosaidia kutoa elimu kwa wananchi.

“Ni kweli wananchi wamekuwa wakinunua Majokofu ya mtumba ambayo yameonekana kuwa na madhara na hiyo yote inatokana na kutokuwa na uelewa juu ya madhara hayo lakini sasa kama tutakuwa na jukwaa la pamoja la kutoa elimu juu ya madhara ya bidhaa hizi za mtumba ninaimani bidhaa hizo za mtumba hazitanunuliwa,” amesema Mwema.

Naye, Fundi anayejishughulisha na Ufundi wa Viyoyozi Matukuta Juma amesema kutokana na ushauri huo   watahamasisha wengine kutumia mitungi ya gesi inayokubalika  huku akitumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuwapunguzia gesi ambayo haiharibu mazingira kwani inauwza bei ya juu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles