26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Jafo awataka viongozi wa dini kuombea mambo machafu machafu

Elizabeth Joachim

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani  Jafo, amewataka viongozi wa dini wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Abuubakar Zubeiry, kuombea baadhi ya mambo machafu machafu yanayoendelea nchini.

Jafo ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 20, akimwakilisha Rais Magufuli katika Baraza Kuu la Maulidi ambalo kitaifa limefanyika Korogwe, mkoani Tanga.

“Mambo hayo machafu machafu yanayoendelea kufanyika nchini na kusababisha mmonyoko wa maadili hayana budi kuombewa,” amesema Jafo.

Aidha, jafo pia amewataka viongozi hao kuendelea kumuombea Rais John Magufuli, ili aendelee kuleta maendeleo ya nchi hasa katika suala la elimu , miundombinu, viwanda na katika sekta ya afya.

“Maendeleo yaliyopo katika nchi yetu si watu wote wanapenda, kuna wengine wanapenda yaharibike lakini kupitia dua zenu mambo yataenda sawa.

“Mwaka 2015 kuelekea 2016 kulitokea tatizo la ukame ambalo lilisababisha mifugo mingi kufa lakini ndani ya miaka mitatu ya serikali ya Rais Magufuli tatizo hilo limekwisha hii ni moja ya maendeleo,” amesema Jafo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles