30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

BoT yafafanua operesheni ya kushtukiza maduka ya fedha Arusha

Mwandishi Wetu, Arusha

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imetoa ufafanuzi kuhusu oparesheni ya kushtukiza ya kukagua maduka ya ubadilishaji fedha ambayo ilizua taharuki jijini hapa jana.

Wanachi jijini arusha walipatwa na taharuki hiyo baada ya maofisa wa serikali wakishirikiana na wanajeshi waliovalia sare na silaha wakipita katika maduka hayo katika operesheni hiyo maalumu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Jumanne Novemba 20, Gavana wa BoT, Profesa Florens Luoga, amesema

operesheni hiyo maalumu kwa ajili ya kukagua maduka bubu ambayo hayana leseni lakini yalikuwa yakiendesha biashara hiyo kinyume na sheria.

“Zoezi hili liliratibiwa na Kitengo cha Ukaguzi cha Benki Kuu katika kutekeleza majukumu yake kisheria, ni oparesheni ya tatu kufanyika na imefanyika baada ya kugundua kuna mtandao mkubwa lakini pia ilionekana inahitajika ushiriki wa maofisa wengi zaidi.

“Uchunguzi wa kina katika miezi sita iliyopita ulibaini kuongezeka kwa biashara za kubadilisha fedha kinyume cha sheria, na kukua kwa biashara haramu ya fedha za kigeni na utakatishaji fedha, hususani kupitia maduka ya kubadilisha fedha,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles