27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Jafo akerwa na viongozi wanaobeza matumizi ya “Force Account”

Na Angela Msimbira, TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo ameonyesha kukerwa na kitendo cha baadhi ya watendaji wa Serikali kukashifu/kudharau matumizi ya mfumo wa ‘Force Account’ kwenye masuala mbalimbali ikiwemo ununuzi wa vifaa kwenye majengo ya Serikali.

Hali hiyo ameinyesha leo Desemba 19, jijini Dodoma wakati alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Hospitali ya Uhuru ambayo imekamilika kwa asilimia 99 huku zikibaki hatua ndogondogo za umaliziaji

Kero hiyo ya Waziri Jafo ilitokana na Mkuu wa Mkoa Dk. Binnilith Mahenge kumweleza kuwa Mkandarasi kutoka Kampuni ya Suma JKT ambao ni watekelezaji wa mradi huo kueleza kuwa baadhi ya vifaa vimechelewa kuwekwa kutokana na gharama zake kuwa juu.

“Unaenda SumaJKT unakuta milioni moja na laki nne, unaenda Don Bosco kule milioni moja na laki mbili lakini unaenda kwenye masoko unakuta laki sita na nusu halafu unasema taratibu za manunuzi, hii haikubaliki katika utendaji nakuagiza Mkurugenzi nenda kanunue vifaa kwa gharama ya soko,”amesisitiza Waziri Jafo.

Waziri Jafo ameeleza kuwa anakerwa na baadhi ya watu wakiwemo viongozi wanaokashifu utaratibu wa Force Account; “Unaondoka Site unakuta kitu laki sita lalafu huku unapata milioni moja na lakini nne au mbili kwa nini usiende kununua pale pa bei rahisi?,” amehoji Jafo.

Waziri Jafo amefafanua kuwa Rais Dk. John Magufuli amejenga vituo vya afya 487 kwa utaratibu wa Force Account na kwamba mwanzo kwa kutumia kandarasi za mwanzo majengo yalikuwa yalijengwa kwa fedha nyingi na gharama kubwa.

”Naomba na viongozi wenzangu wengine mnaokaa mnakashifu utaratibu wa Force Account msiongopewe hivi hamfikirii zamani jengo la Bilioni mbili leo linajengwa kwa bei ndogo halafu leo watu wanasimama wanasema utaratibu huu hauna maana unajua kuna watu wa ajabu sana na inawezekana wengine hawajui maisha halisi ya watanzania huu utaratibu umetusaidia shule kongwe zimekarabatiwa,”amesema Jafo.

Awali, Dk. Mahenge alimweleza Waziri huyo kuwa mradi huo ulikuwa uwe umekamilika lakini kuna changamoto ya baadhi ya fedha ambazo bado hazijatolewa

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles