26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Jafo afurahishwa kasi ya ujenzi Hospitali Kilolo

RAYMOND MINJA IRINGA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo amekoshwa  na kasi ya ujenzi wa hospitali ya kisasa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa ambayo itakuwa ni mkombozi mkubwa kwa wakazi wa kilolo waliokuwa wakipoteza maisha kwa kufuata huduma umbali mrefu.

Akizungumza mara baada ya  kukagua hospitali hiyo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya  kukagua miradi inayotekelezwa na Serekali, Jafo amesema kuwa moja ya miradi bora na yenye majengo yaliyoridhisha ni pamoja na hospitali ya kilolo.

“Ndugu zangu katika hospitali bora kabisa zinazojengwa hii ni moja wapo, viongozi wa wilaya na mkoa mmefanya kazi kubwa sana kwa kusimamia ujenzi huu mimi nimeridhishwa kabisa na ubora wa majengo haya hongereni sana “amesema.

Aidha amewataka viongozi  hao kuhakikisha wanawasimamia wakandarasi wa majengo hayo kumalizia vizuri ili kuondokana na kasoro ndogo ndogo ambazo ambazo ameziona  hasa kwenye milango ili wazirekebishe.

“Nimetembea kwenye majengo haya yamejengwa vizuri kwa kufuata vigezo stahili lakini tatizo ambalo nimelibaini ni kuwa milango haijakaa vizuri inahitajika kutolewa na kuwekwa milango mipya hivyo naombeni hakikisheni mnasimamia ili tusiharibu thamani kubwa na uzuri wa majengo kwa kushindwa kumalizia kazi vizuri” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles