26.1 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Jaden Smith amtambulisha mpenzi wake

Snip20150915_13NEW YORK, MAREKANI

CHIPUKIZI wa filamu nchini Marekani, Jaden Smith, ameonesha watu kuwa amekua baada ya kumtambulisha
mpenzi wake, Sarah Snyder.

Msanii huyo mwenye miaka 17, aliambatana na mpenzi wake huyo katika maonyesho ya Gypsy Sport juzi jijini New York.

Uhusiano wa wawili hao ulianza mwanzoni mwa Julai, mwaka huu, baada ya kuonekana wakiwa
pamoja katika matukio mbalimbali.

Awali msanii huyo alidaiwa kuwa na uhusiano na mpenzi wa msanii wa Hip Hop, Tyga, Kylie Jenner, kabla ya kutoka na Amandla Stenberg, Mei mwaka huu.

“Nadhani huu ni wakati wangu sahihi wa kufanya kile ambacho ninakitaka,” alisema Smith. Hata hivyo, baba wa msanii huyo, Will Smith aliwahi kusema kuwa hawezi kumuachia mtoto wake aanze kufanya mambo yake
kabla ya kufikisha miaka 18.

Mtoto huyo akiwa na umri wa miaka 15 alimuomba baba yake aishi kwenye nyumba yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles