25.3 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Ja Rule amshangaa 50 Cent

NEW YORK, MAREKANI



RAPA Jeffrey Atkins maarufu kwa jina la Ja Rule, amemshangaa 50 Cent kwa kitendo chake cha kununua tiketi za watu 200 wa siti za mbele ili ziwe wazi katika shoo yake mapema mwezi huu.

Ja Rule anatarajia kufanya shoo yake Novemba 9 mwaka huu, hivyo 50 Cent ameamua kununua siti 200 zote za mbele ili ziwe wazi kwa ajili ya kumuharibia msanii huyo.

Wawili hao wamekuwa kwenye mgogoro kwa kipindi cha miaka 20 sasa, hivyo kitendo hicho kinaonesha hakuna dalili za kumaliza tofauti zao.

Kupitia ukurasa wa Instagram Ja Rule aliandika na kudai kitendo alichokifanya 50 kinamshangaza lakini amekipenda.
“Nimependa kitendo ulichokifanya, siku zote nipo juu yako na ninachokiangalia ni jinsi gani nitapata fedha,” aliandika Ja Rule.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles