24.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

IRAN KUBORESHA MAKOMBORA KUIKABILI MAREKANI

TEHRAN, IRAN

BUNGE la Iran limepitisha muswada wa kutenga zaidi ya dola nusu bilioni kwa ajili ya mradi wa kuboresha makombora ili kukabiliana na ubabe wa Marekani.

Hatua hiyo ya Iran inajibu vikwazo vya karibuni kabisa vilivyowekwa na Marekani dhidi ya nchi hiyo.

Vyombo vya habari vya taifa vinasema, fedha hizo pia zinakusudiwa kupambana na vile walichosema vitendo vya kigaidi vya Marekani katika Mashariki ya Kati.

Muswada huo utaweka vikwazo dhidi ya wanajeshi pamoja na maafisa wa ujasusi wa Marekani.

Mpatanishi mkuu wa Iran katika mazungumzo kuhusu mradi wake wa nyuklia, Abbas Araqchi, amesema, muswada huo mpya, umeungwa mkono na wizara ya mambo ya nje, na kwamba hauendi kinyume na makubaliano ya mwaka 2015, yaliyozuia mradi wa nyuklia wa Iran.

Makubaliano kuhusu programu ya nyuklia kati ya Iran na mataifa sita yenye nguvu duniani ikiwemo China, Urusi na Uingereza, yamelenga kuizuia Iran kuunda zana za nyuklia.

Makubaliano hayo yalisababisha vikwazo vibaya kwa uchumi wa Iran kuondolewa, ili nchi hiyo ipate kupunguza programu zake za nyuklia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles