24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Infinix, Tigo wazindua rasmi Infinix Hot 12 na Infinix Hot 12 Play Tanzania

*Wateja kupata 78GB za Intaneti bure mwaka mzima

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Kampuni ya simu za mkononi Infinix, kwa kushirikiana na kampuni ya Tigo Tanzania imezindua simu za Infinix HOT 12 na Infinix HOT 12play ikiwa ni muendelezo wa toleo la series ya Infinix HOT.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyia leo Dar es Salaam Mei 11, 2022, Afisa Uhusiano wa Infinix, Aisha Karupa amesema wanafurahi kuzindua bidhaa hiyo nakwmaba ni simu ya kisasa inayotoa urahisi kubwa kwa mtumiaji wake.

“Tunafuraha kuzindua Modeli ya kwanza ya Infinix kutoka mfululizo wa HOT itakayokuwa na chipset ya G85 ya games, Infinix Hot 12 ni simu bora na nyepesi zaidi kwa upande wa game ambapo mtumiaji anaweza kucheza gemu lake bila kugandaganda na huku akiendelea kuwasiliana katika mitandao mingine ya kijamii.

“Pia ina ubora wa juu zaidi wa betri, Infinix HOT 12 ina vifaa vya 5000mAh, chaji ya hali ya juu ya Type -C18W, teknolojia ya kudumu ya betri ya Infinix iliyojitengenezea ambayo hufanya betri ikae na chaji kwa muda mrefu sana, ambapo chaji 5% inaweza kukaa na kutumika kwa hadi masaa 2.6.

“Infinix HOT 12 ina mwonekano wa kuvutia na skrini ya inchi 6.82” ya 90Hz Pro-Level ya esports kwa ingizo laini la silky-laini na sampuli ya mguso 180Hz inayoipa Infinix HOT 12 kiwango cha mwitikio cha haraka ambacho ni bora kabisa kwa games, Infinix HOT 12 sasa inapatikana katika maduka yote ya simu nchini Tanzania ikiwa na ofa ya GB78,” amesema Aisha.

Naye kwa upande wake Mtaalam wa Vifaa vya Intaneti kutoka Tigo, Blass Abdon amesema kuzinduliwa kwa simu hizo katika soko la Tanzania kutaongeza thamani katika mazingira ya biashara na kuboresha maisha ya Watanzania nakwamba utapunguza mgawanyiko wa kidijitali kwa kuongeza matumizi ya simu janja nchini.

“Kama sehemu ya mkakati wetu endelevu wa kuimarisha upenyezaji na matumizi ya simu za kisasa za mtandao wa Tigo 4G nchini, tunaendelea kuungana na Infinix Tanzania ili kuhakikisha wateja wetu na Watanzania kwa ujumla wanapata huduma iliyo bora hasa kupitia simu janja zinazowezeshwa 4G. Leo tumezindua simu mbili za kisasa zaidi sokoni na wateja wetu kote nchini wataweza kutumia mtandao wa Tigo 4G na simu hizi za kisasa,” amesema Abdon.

Kwa mujibu wa Abdon simu hizi zitapatikana katika maduka yote ya Tigo nchini pia zitakuja na bando la data la 78GB BURE kwa mwaka mzima.

Ikumbukwe kuwa mwendelezo (Series) wa HOT tangu kutambulishwa kwake haijawahi kuja na processor ya speed ya juu zaidi kuizidi Infinix HOT 12 na hii kuifanya Infinix HOT 12 kuwa toleo muhimu sana kwa kampuni ya Infinix na wateja wa simu za Infinix.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles