23.8 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kujenga daraja lililobomoka miaka 8 iliyopita

Na Denis Sinkonde, Songwe

Wananchi wa Kijiji cha Ilanga Kata ya Mlale wilayani Ileje mkoani Songwe wameiomba Serikali kuwajengea daraja la mto Isenga linalotenganisha vijiji vya Ilanga wilayani ya Ileje na Namwangwa wilayani Mbozi ili kuondoa adha wanayoipata.

Kaimu Meneja wa TARURA wilayani Ileje, Mhandisi Pakibanja.

Kwa mujibu wa wananchi hao daraja hilo liliharibiwa na mvua miaka 8 iliyopita ambapo hadi sasa watu wanne wamefariki dunia kutokana na daraja hilo huku 18 wakinusurika kufa maji pindi mvua kubwa zinaponyesha.

Wananchi hao walitoa ombi hilo kwa mkuu wa Wilaya hiyo, Anna Gidarya wakati wa ziara ya kusikiliza kero za wananchi katika kata ya Mlale ambapo wananchi hao wamesema daraja hilo liliharibika miaka 8 iliyopita.

Mkazi wa kijiji cha Mlale kata ya Mlale wilayani Ileje, Wokovu Mwazembe amesema daraja  hilo ni kiunganishi muhimu baina ya vijijini hivyo hivyo ni muhimu serikali kutatua changamoto hiyo ambayo imepoteza nguvu kazi kwa taifa.

Daraja hilo ni kiunganishi muhimu kwa wananchi wa wilaya hiyo katika shughuli za kilimo na kibiasha kwani huishi kwa kutegemeana ikiwepo baadhi ya wanafunzi kusoma shule ya msingi Ilanga iliyopo kijiji cha Ilanga wilaya ya Ileje hivyo wameiomba serikali kuwajengea daraja hilo,” amesema Wokovu.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Mfano Kayuni amekili kuwepo kwa changamoto hiyo tangu daraja hilo kuvunjika miaka 8 iliyopita hali ambayo imeathiri uchumi wa wananchi wa vijiji hivyo ambao hutegemea uzalishaji wa mazao Kwa kuvusha kupitia daraja hilo.

Diwani wa kata hiyo, Yotamu Ndile amesema daraja hilo limekuwa kero kwa shughuli za wananchi ambao baadhi Yao hulima mashamba upande wa Mbozi wengine Ileje.

“Tangu daraja hilo kubomoka wananchi wanashindwa kusafirisha shughuli mazao yao kipindi cha mavuno na kipindi masika watu zaidi ya 4 wamefariki na wengine 18 kuokolewa kipindi cha masika wakitaka kuvuka wakitoka katika shughuli za shamba,” amesema Ndile.

Akijibu kero hiyo kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) wilayani Ileje, Mhandisi Pakibanja amesema tayari serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 imetenga jumla ya Sh milioni 100 kwa ajili ya upembuzi yanikifu kwa madaraja mawili ambayo ni korofi katika kata hiyo ambalo ni daraja la mto Isenga katika Kijiji cha Ilanga na daraja la Mto Mafumbo hivyo kila daraja limetengewa Sh milioni 50.

“Serikali inatambia adha wanayokumbana nayo wananchi tangu kubomoka Kwa daraja hilo hivyo tunatarajia kupata upembuzi yakinifu ili kwa gharama ya Sh 50,000,000 kwa kila daraja, hivyo wananchi wawe wavumilivu,” amesema Mhandisi Pakibanja.

Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Anna Gidarya amewataka wananchi kuendelea kutunza miundombinu inayojengwa na serikali ili kuwanufaisha wananchi waliowengi ikiwa ni pamoja na kuwarahisishia usafiri utokanao na barabara pamoja na madaraja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles