27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

INFINIX NOTE 30 yajizolea sifa Kimataifa 2023

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Chapa ya Simu mahiri inayoongoza kwa ubora  Infinix Mobile LTD imegonga vichwa vya habari wiki hii baada ya Infinix NOTE 30 kushinda Tuzo mbili ya Usanifu wa bidhaa/Vyombo vya habari na Tuzo ya Electroniki za nyumbani zinazoandaliwa kila mwaka Paris nchini Ufaransa.

NOTE 30 imeundwa kukidhi mahitaji ya mitandao ya simu za mkononi ndani na nje ya nchi.

Tuzo hizo zinazofahamika kama Paris Design hutoa heshima katika taaluma ya Usanifu, usanifu wa ndani, Usanifu wa mandhari, usanifu wa picha na usanifu wa bidhaa ikitunuku mbunifu bora zaidi duniani kote.

“Hii ni heshima kubwa kwetu kama kampuni ambayo inakuwa kwa kasi kubwa inayotokana na uzalishaji wa bidhaa zenye teknolojia ya hali ya juu kwa gharama nafuu,” imeeleza kampuni hiyo.

Tanzania ni moja ya nchi ambayo inanufaika vyema na bidhaa za kampuni hiyo, imekuwa na mchango mkubwa katika kufanya teknolojia ya mawasiliano kupitia njia ya simu kuenea kwa wepesi.

Hii siyo mara ya kwanza kwa kampuni hii kushinda tuzo hizo za kimataifa mwaka 2021 pia ilitwaa tuzo ya bidhaa yenye nidhamu katika kitengo cha mawasiliano huko barani Asia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles