21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

FCC kuendesha kazi kwa njia ya mtandao

Na Mwandishi wetu, Dodoma

KATIKA Mwaka wa Fedha 2023/24 Tume ya Ushindani (FCC) imepanga kuanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Uendeshaji wa Shughuli za tume hiyo uitwao (FCC – MIS).

Hayo yameelezwa jijini Dodoma leo Jumatano Agosti 2,2023 na Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, William Erio wakati akiwasilisha kwa Waandishi wa Habari kuhusu utekelezaji wa Tume hiyo na mwelekeo kwa mwaka 2023-24.

Erio amesema mfumo huo utaongeza ufanisi wa FCC kwa kusogeza huduma kwa wateja.

Amezitaja huduma zitakazonufaika na mfumo huo ni pamoja na Uidhinishaji wa Miungano ya Kampuni (Merger Clearance Process) Uidhinishaji wa maombi ya makubaliano maalum (Exemption of Agreement).

Pia kusajili mikataba ya huduma kwa mteja (Standard form Consumer Contract Registration) fomu zinazohusika na utekelezaji wa sheria ya alama za bidhaa.

“Hii ni kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara na Serikali kwa ujumla ili kuhakikisha kuwa michakato wa marekebisho ya (FCA) na ile ya Alama za Bidhaa (MMA) inakamilika,”amesema Erio.

Vilevile ametaja mipango mingine kuwa ni kuimarisha Ofisi za Kanda ikiwa ni pamoja na kuanzishaoOfisi mbili mpya za kanda katika Mikoa ya Tanga na Mtwara ili kusogeza huduma karibu na wananchi, hivyo kutasababisha ofisi za Kanda kuwa sita (6).

Pia kufanya tatifi mbili za ushindani kuhusu soko la nyaya za umeme wa matumizi ya nyumbani na soko la pareto.

Pia kuendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya ushindani, kuwalinda walaji na udhibiti wa bidhaa bandia kupokea na kuchunguza miungano ya kampuni na kuchunguza na kukamilisha mashauri yanayohusu mienendo ya upangaji njama na matumizi mabaya ya nguvu ya soko.

“Kuendeleza jitihada za kumlinda mlaji wa bidhaa na huduma na kuendeleza udhibiti wa bidhaa bandia,”amesema Mkurugenzi huyo.

Katika hatua nyingine amesema kuwa wamepokea malalamiko 58 ya watumiaji wa bidhaa na huduma yanayohusu mikataba inayoandaliwa na upande mmoja usalama wa bidhaa, upotoshaji katika bidhaa, huduma za kifedha na huduma za bima.

Amesema utekelezaji ni malalamiko 21 yaliyohusu masharti ya mikataba inayoandaliwa upande mmoja yalipatiwa ufumbuzi.

“Malalamiko yaliyohusu upotoshaji wa bidhaa yalipatiwa ufumbuzi, malalamiko 13 yaliyohusu huduma za fedha, usalama wa bidhaa na huduma na bima ambayo yalihamishiwa katika Mamlaka sahihi ambazo ni TBS, BOT na Jeshi la Polisi.

“Malalamiko 19 yako katika hatua mbalimbali za kupatiwa ufumbuzi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles