25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Ikungi kinara ujenzi wa madarasa Singida

*Wakabidhi rasmi vyumba 29

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba amepokea madarasa 29 yenye thamani ya Sh milioni 580 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Jerry Muro ikiwa ni utekelezaji wa agizo lake la kuwataka wakuu wa wilaya kukabidhi vyumba vipya vya madarasa.

Akizungumza leo Desemba 15, 2022 wakati wa makabishiano hayo Serukamba amesema wilaya ya Ikungi imekuwa ya kwanza kwa vipindi viwili mfululizo kumaliza miradi ya ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa kwa mkoa.

Aidha, amempongeza mkuu wa wilaya ya Ikungi, Muro na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ikungi, Justice Kijazi na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ali Mwanga kwa kusimamia kikamilifu ujenzi wa madarasa hayo ambayo yamekuwa na kiwango bora kinachoendana na thamani ya fedha

Akikabidhi madarasa hayo katika hafla iliyofanyika katika shule ya Sekondari ya Isuna, Muro amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia wilaya ya Ikungi kupewa Sh milioni 580 na kusisitiza kukamilika kwa madarasa hayo kunatoa fursa ya kuanza maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mapema mwezi Januari mwaka 2023.

Pia amesisitiza katika wilaya ya Ikungi hakuna mwanafunzi atakaepangiwa katika shule za Ikungi atakosa darasa na kiti na meza mana wameshakamilisha pia uwekaji wa viti 1,160 pamoja na meza zake umekamilika kwa shule zote 16 na kilichopo ni wazazi kuandaa watoto.

Wakiongea kwa niaba ya wananchi Mbunge wa jimbo la singida mashariki, Miraji Mtaturu pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya ikungi wamewataka wananchi kujiandaa kutumia miundombinu hiyo vizuri kwa kupeleka watoto shule pamoja na kulinda na kutunza miundombinu hiyo uku wakiendelea kumuomba Rais, Dk. Samia kuleta fedha zingine za miradi kutokana na miradi kusimamiwa vizuri Ikungi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles