24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

IFM kuwapiga msasa watumishi Simiyu

Na Derick Milton, Simiyu

Uongozi wa Mkoa wa Simiyu na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wameingia makubaliano ya kuwajengea uwezo watumishi wa serikali katika mkoa huo kwenye Halmashauri zake  sita, taasisi za umma  na wafanyabiashara wakiwamo wajasliamali.

Hati ya makubaliano hayo  ya miaka mitano, imesainiwa leo  Alhamisi Agosti 12  kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa kati ya Katibu Tawala wa mkoa hu, Prisca Kayombo na Mkuu wa Chuo cha IFM, Profesa Thadeo Satta, ambapo makubaliano hayo ya miaka mitano.

Akizungumza baada ya kusainiwa kwa hati hiyo, Prisca amesema kuwa wazo la kutumia chuo cha IFM kuwajengea uwezo watumishi wa mkoa huo lilitolewa na Mkuu wa Mkoa David Kafulila kutokana na chuo hicho kuanzisha tawi lake Simiyu.

Amesema kuwa mkuu wa mkoa wakati akitoa wazo hilo, alisema uwepo wa chuo hicho katika mkoa wake ni fursa kubwa hasa kuwajengea uwezo watumishi wake katika eneo la ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa halmashauri, usimamizi wa matumizi sahihi ya fedha pamoja na kusaidia kubuni vyanzo vipya vya mapato.

Amesema kuwa chuo cha IFM kimekuwa na watalaamu wabobezi katika mambo ya fedha, pamoja na kufanya tafiti mbalimbali katika eneo hilo, hivyo kupitia makubaliano hayo watumishi wa mkoa huo watajengewa uwezo wakutosha ili kuwaletea wananchi maendeleo.

” Lengo kubwa la makubaliano haya, tunataka watumishi wa Halmashauri zetu wajengewe uwezo wa kukusanya mapato, matumizi sahihi ya fedha za umma, lakini pia kuwajengea uwezo wa namna ya kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kuwaletea maendeleo wananchi,” amesema Prisca.

Naye Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu Mkoa, Donatus Weginah, amesema  makubaliano hayo yatahusu pia  taasisi nyingine za umma zilizopo mkoani humo, wafanyabiashara na  wajasliamali.

Weginah ameeleza kuwa katika mkoa huo wafanyabiashara wengi hawana tabia ya kutunza kumbukumbu za biashara zao, licha ya kumiliki au kufanya biashara kubwa, ambapo kupitia makubaliano hayo nao watanufaika.

Kwa upande wake Profesa Satta, ameupongeza Mkoa wa Simiyu kwa kubuni jambo hilo, ambalo ameeleza limefanya chuo hicho kuwa cha kwanza nchini kati ya vyuo vyote kuingia makubaliano na serikali ya kuwajengea uwezo watumishi wa umma.

Profesa Satta amesema kuwa tangu kuzinduliwa kwa tawi la Sapiwi la chuo hicho Simiyu, jumla ya wanafunzi 107 wameanza masomo ambapo asilimia kubwa wanatoka katika mkoa huo.

” Tunatumaini kupitia makubaliano haya, watumishi watapata fursa ya kuongeza ujuzi na maarifa katika majukumu yao, na sisi kama chuo wiki ijayo tutaanza kuzifikia halmashauri kwa ajili ya kuzungumza nao kujua ni maeneo gani wanataka kujengewa uwezo,” amesema Profesa Satta.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa huo, Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge amemtaka Katibu tawala mkoa kuhakikisha anawasimamia wakurugenzi wa halmashauri zote kushiriki kikamilifu katika makubaliano hayo ili watumishi wajengewe uwezo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles